• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa UM asisitiza umuhimu wa maendeleo katika kukabiliana na suala la wakimbizi barani Afrika

    (GMT+08:00) 2019-05-24 08:57:02

    Ofisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa amesisitiza umuhimu wa maendeleo katika kukabiliana na suala la wakimbizi barani Afrika.

    Akizungumza kwenye mkutano wa vyombo vya habari kuhusu Afrika, naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa na mshauri maalumu kuhusu mambo ya Afrika Bience Gawanas ametoa wito wa kuongeza uwekezaji katika maendeleo ya Afrika, ili watu wa Afrika waweze kupata huduma na mahitaji ya kimsingi ikiwemo elimu, huduma za afya, maji na usafi. Ameongeza kuwa Umoja wa mataifa utahakikisha kuwa Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Umoja huo yanawanufaisha watu wa Afrika, haswa wale waliolazimishwa kukimbia makwao.

    Takwimu zinaonesha kuwa, mpaka mwezi Juni mwaka 2018, Afrika imeshuhudia wakimbizi na watu wanaotafuta hifadhi milioni 6.2, na wakimbizi wa ndani milioni 15.5.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako