• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa waimarisha hatua za kukabiliana na Ebola nchini DRC

  (GMT+08:00) 2019-05-24 08:57:23

  Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema Umoja huo unaimarisha hatua zake za kukabiliana na mlipuko wa homa ya Ebola nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo DRC, ambao umesababisha vifo vya watu zaidi ya 1,200 tangu ulipoibuka mwezi Agosti mwaka jana.

  Amesema katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ameanzisha utaratibu imara wa uratibu na uungaji mkono katika eneo la Butemba ulipotokea mlipuko wa Ebola, na kumteua naibu mkuu wa tume ya Umoja huo Bw. David Gressly kuwa mratibu wa hatua za dharura za kupambana na Ebola.

  Bw. Dujarric amesema Bw. Gressly atasimamia uratibu wa uungaji mkono wa kimataifa katika kukabiliana na homa ya Ebola, na kuhakikisha kuwa mazingira wezeshi, haswa kwa upande wa kiusalama na kisiasa, yanapatikana ili kuongeza ufanisi wa hatua za kukabiliana na homa hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako