• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa UM atoa wito wa kufuata kanuni za vita ili kuwalinda raia

  (GMT+08:00) 2019-05-24 09:53:47

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres ametoa wito wa kufuata kanuni za vita ili kulinda raia, na ameeleza kusikitishwa na ukweli kwamba ulinzi wa raia unazidi kuzorota.

  Akihutubia mjadala wa wazi wa Baraza la Usalama la Umoja huo Bw. Guterres amesema, changamoto kuu ni kuhakikisha sheria ya kimataifa ya kibinadamu inaheshimiwa na kufuatwa, lakini mara kwa mara, sheria hiyo haifuatwi kikamilifu, na hata baadhi ya wakati inakiukwa.

  Amesema mwaka jana, Umoja wa Mataifa umerekodi vifo na majeruhi ya raia 22,800 katika nchi sita za Afghanistan, Iraq, Mali, Somalia, Sudan Kusini na Yemen.

  Naye mjumbe wa kudumu wa China katika umoja huo Balozi Ma Zhaoxu ameitaka jumuiya ya kimataifa ifanye juhudi kuwalinda raia katika mapambano. Amesema kuzuia na kutatua migogoro kwa njia ya amani ni mbinu bora zaidi ya kuwalinda watu wa kawaida.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako