• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa China atuma salamu za pongezi kwa waziri mkuu wa India baada ya chama chake kushinda katika uchaguzi

  (GMT+08:00) 2019-05-24 10:21:12

  Rais wa China Xi Jinping ametuma salamu za pongezi kwa Waziri mkuu wa India Narendra Modi baada ya chama chake cha Bharatiya Janata BJP kushinda kwenye uchaguzi. Programu ya simu ya mkononi ya Tume ya Uchaguzi ya India ECI imetangaza ushindi wa chama cha BJP katika uchaguzi mkuu wa 17 uliomalizika hivi karibuni. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ECI, chama hicho kimepata kura 272, idadi ambayo imefikia kigezo cha nusu ya kura zote cha kuanzisha serikali. Kura za chama hicho zinaonekana kuendelea kuongezeka, wakati wagombea wa chama hicho wakiongoza katika majimbo 31 zaidi ya bunge. Kura bado zinaendelea kuhesabiwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako