• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu mkuu wa UN alaani mashambulizi ya watu wenye silaha dhidi ya vijiji Jamhuri ya Afrika ya Kati

    (GMT+08:00) 2019-05-24 16:47:40

    Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres amelaani vikali mashambulizi dhidi ya vijiji yaliyofanywa kaskazini magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati na watu wenye silaha na kusababisha vifo vya watu 34.

    Taarifa aliyotoa kupitia msemaji wake Bw. Stephen Dujarric imesema, mashambulizi hayo kwenye vijiji kadhaa karibu na mpaka na Chad yamefanywa na kundi la 3R ambalo lilisaini makubaliano ya kusimamisha vita Februari 6 mjini Bangui.

    Bw. Guterres ameitaka mamlaka nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati kufanya uchunguzi kuhusu mashambulizi hayo na kuwafikisha wahusika mbele ya sheria haraka iwezekanavyo, na kusema mashambulizi dhidi ya raia ni uhalifu wa kivita. Amezitaka pande zote zilizosaini makubaliano ya amani kuacha matumizi ya mabavu kutokana na wajibu wa utekelezaji wa makubaliano hayo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako