• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yataka kuondoa mzizi wa tatizo la kuwalinda raia kwenye mapambano

  (GMT+08:00) 2019-05-24 16:52:47

  Balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu jana alihudhuria mkutano wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa juu ya suala la kuwalinda raia kwenye mapambano, akitaka kuimarisha kuzuia mapambano, na kuondoa mzizi wa tatizo la kuwalinda raia kwenye maeneo ya mapambano.

  Amesema mwaka huu inatimia miaka 70 tangu Mkataba wa Geneva upitishwe, pia inatimia miaka 20 tangu Ajenda ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ya kuwalinda raia walioko kwenye mapambano ianzishwe. Hata hivyo, hali ya usalama ya dunia bado sio nzuri, raia wengi wanauawa au kujeruhiwa kwenye mapambano. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linapaswa kutekeleza wajibu wa kwanza katika kulinda amani na usalama duniani, na kutatua mapambano kwa njia ya mazungumzo.

  Wakati huo huo, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres jana ameonya kuwa ingawa mfumo wa sheria ya kibinadamu ya kimataifa unaendelea kukamilishwa, hali ya kuwalinda raia walioko kwenye mapambano inazidi kuwa mbaya. Ametoa wito kwa nchi wanachama ziweke mfumo wa kuwalinda raia hao na kuanzisha idara maalumu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako