• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wataalamu wasema lawama ya Marekani kuhusu "China kulazimisha kuuza teknolojia" haina msingi wowote

    (GMT+08:00) 2019-05-24 17:32:23

    Tangu Marekani ianzishe mvutano wa kibiashara kati yake na China mwaka jana, Marekani imedai mara kwa mara kuwa China inalazimisha kuuza teknolojia. Wataalamu wa China wamesema, lawama hiyo ni kisingizio cha kuzuia maendeleo ya China, na haina msingi wowote. Wakati huohuo, wataalamu hao wamesema, nguvu ya China katika kulinda hakimiliki ya ubunifu inazidi kuimarishwa, huku China ikiyachukilia kwa usawa makampuni mbalimbali, yakiwemo makampuni ya nchi za nje.

    Mchumi maarufu wa China ambaye pia ni mkuu wa heshima wa taasisi ya maendeleo ya taifa ya Chuo Kikuu cha Peking Bw. Lin Yifu amesema, makampuni ya nchi za nje kuleta ufundi katika soko la China ni chaguo la lazima la ushindani wa soko. Anasema,

    "Makampuni ya Marekani yakija kuwekeza nchini China, lazima yaje na teknolojia zao. Kuja na teknolojia zao kumelazimishwa na China? Hapana. Kwa sababu kama yakitaka kutengeneza bidhaa nchini China na kuingia katika soko la China, bidhaa zao hazitakuwa na nguvu ya ushindani bila ya kutumia teknolojia bora. Kwa mfano magari, China imekuwa nchi inayotengeneza magari mengi zaidi duniani, na pia ni soko kubwa zaidi la magari. Mbali na makampuni ya magari ya Marekani, makampuni ya Ujerumani, Japani, Korea Kusini pia yameanzisha shughuli zao nchini China. Kama makampuni ya General Motors na Ford ya Marekani hayatatumia teknolojia nzuri zaidi nchini China, magari yao hayatanunuliwa na wateja. Tunajua kwamba makampuni hayo yanatengeneza magari mengi zaidi nchini China kuliko nchini Marekani, na faida yao kubwa inatokana na China. Hivyo kutumia teknolojia nzuri zaidi katika soko la China ni chaguo lao, wala si kulazimishwa na serikali ya China. Kama makampuni hayo yakilazimishwa, wanaweza kuchagua kutokuja China. "

    Wataalamu wamesema, China siku zote inatilia maanani katika uwezo wa uvumbuzi. Tangu mwaka 2000, gharama ya utafiti wa jamii nzima ya China inaongezeka kwa asilimia 20 kila mwaka. Wakati huohuo, China pia inaimarisha ulinzi wa hakimiliki ya ubunifu. Tangu mwaka 2001, malipo yanayolipwa na China kwa hakimiliki za ujuzi za nje yanaongezeka kwa asilimia 17 kwa mwaka.

    Mkurugenzi wa ofisi ya utafiti wa biashara ya kimataifa kwenye taasisi ya sayansi za kijamii ya China Bibi Dong Yan anaona kuwa kufuatia ongezeko la ushindani la makampuni ya China na mabadiliko ya soko la China, madai ya Marekani yasiyo na msingi dhidi ya China pia yanatokana na sababu ya kiuchumi. Bibi Dong anasema,

    "Ukweli ni kwamba hatuna sheria yoyote kuhusu kulazimisha kuuza teknolojia. Madai hayo yameonesha kuwa katika mchakato wa makampuni ya Marekani kuwekeza nchini China na mchakato wa mabadiliko ya uchumi wa China, makampuni hayo yanakabiliwa na mashinikizo kadhaa. Kwa mfano, makampuni mengi ya nchi za nje yalipata nafuu ya kodi na ardhi. Hivi sasa makampuni hayo hayana tena nafuu hiyo, ushindani wa makampuni ya ndani pia unaongezeka, hii imekuwa sababu yao ya kiuchumi kuilaumu China."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako