• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping wa China akutana na makamu wa rais wa Brazil

    (GMT+08:00) 2019-05-24 19:16:06
    Rais Xi Jinping wa China akutana na makamu wa rais wa Brazil

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing alipokutana na makamu wa rais wa Brazil Bw. Hamilton Mourao, amesisitiza kuwa pande hizo mbili zinapaswa kuendelea kuchukuliana kama fursa na mwenzi wa kujiendeleza, na kuujenga uhusiano kati ya pande hizo mbili uwe mfano wa ushirikiano wa mshikamano kati ya nchi zinazoendelea. Kwenye Mazungumzo hayo rais Xi ameeleza kuwa China na Brazil ni nchi kubwa zaidi zinazoendelea duniani, vilevile ni masoko mapya ambayo yana matumaini ya kupata maendeleo kwa pamoja, na zina mustakabali mkubwa wa kujiendeleza. Akisema:

    "China na Brazil ni nchi kubwa zaidi zinazoendelea duniani. Urafiki kati ya pande hizo mbili umekuwa ukidumisha maendeleo yenye utulivu katika muda mrefu uliopita. Mwaka huu ni Maadhimisho ya miaka 45 tangu uhusiano wa kibalozi kati ya pande hizo mbili uanzishwe. Tunatakiwa kujumuisha uzoefu uliopatikana, huku tukitupia macho siku za baadaye, kuendelea kukuza ushirikiano wa kunufaishana, ili kuwanufaisha vizuri zaidi watu wa nchi hizo mbili."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako