• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uchaguzi wa bunge la Ulaya wafanyika nchini Uingereza na Uholanzi

    (GMT+08:00) 2019-05-24 19:53:28

    Uchaguzi wa bunge la Ulaya unaofanyika kila baada ya miaka mitano, utafanyika tarehe 23 hadi 26 mwezi huu katika nchi wanachama 28 wa Umoja wa Ulaya. Wabunge 751 watakaochaguliwa kwa kupigwa kura wataunda bunge la tisa la Ulaya. Jana wapiga kura wa Uingereza na Uholanzi walipiga kura.

    Siku hiyohiyo wagombea 308 wa Uholanzi waligombea viti 26, na matokeo yanaonyesha kuwa chama cha Leba kimepata viti vitano bila ya kutarajiwa na kuwa mshindi mkubwa kabisa kati ya vyama 16 vya siasa vinavyogombea vya Uholanzi.

    Wapiga kura wa Uingereza watachagua wagombea 73 kuingia kwenye bunge la Ulaya. Kutokana na maoni ya watu yaliyofanyika hapo awali, chama cha Brexit kinachoongozwa na Nigel Farage ambaye pia ni kiongozi wa zamani wa chama cha uhuru kinatarajiwa kupata theluthi moja ya viti 73, na kuna uwezekano kwamba chama cha wahafidhina kinachoongozwa cha waziri mkuu wa nchi hiyo Bibi Theresa May kitashindwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako