• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waliouzia NYS bidhaa hawajalipwa miaka 4 baadaye

    (GMT+08:00) 2019-05-24 20:14:32
    Baadhi ya wanakandarasi halali wa Huduma ya Kitaifa ya Vijana nchini Kenya (NYS) kufikia sasa hawajalipwa miaka minne baada ya kutoa bidhaa kwa shirika hilo.

    Huku wanakandarasi haramu wakizidi kufurahia mamilioni waliyopora, wale halali waliotoa bidhaa za ujenzi walisahaulika.

    Wafanyibiashara hao walitoa vifaa vya ujenzi, sehemu za magari, sare, vyakula, vitabu na kalamu na vifaa vya mawasiliano miongoni mwa vifaa vingine.

    Bidhaa na huduma hizo zilitolewa wakati wa awamu ya mwanzo ya programu ya kuwawezesha vijana na mradi wa taa mitaani.

    Baadhi ya wanakandarasi hao waliaga dunia, wengine waliachwa na wachumba, ilhali baadhi yao wanakabiliana na minada, kufurushwa na kufungiwa nyumba, huku wakiorodheshwa kwenye CRB kwa kulemewa kulipa madeni.

    Wafanyabiashara hao wameeleza kuwa kumbukumbu yao ya NYS ni nyaraka zinazotoa ushahidi kuwa walitoa bidhaa na huduma kwa serikali.

    Kulingana na ripoti ya Mkaguzi Mkuu wa Fedha za serikali Edward Ouko, NYS na wizara inayosimamia huduma hiyo haijalipa watoaji huduma na bidhaa kufikia 800 takriban Sh3 bilioni.

    Kwa jumla, wanakandarasi wanadai serikali Sh11.3 bilioni katika biashara zote – halali na haramu.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako