CAG huyo mstaafu alitoa kauli hiyo katika mapitio ya ripoti ya CAG kwa mwaka 2017/2018 kwa wakurugenzi wa mtandao wa asasi za kiraia nchini wa kanda ya kati, katika kikao kilichofanyika jijini hapa.
Alisema ripoti hizo zinaonyesha mapato na matumizi ya fedha za bajeti zilizopitishwa na bunge ambazo kwa kiasi kikubwa zinatokana na walipa kodi, hivyo zinatakiwa kuwa wazi.
Utouh ambaye pia Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Wajibu, alisema ripoti hizo ndilo jicho la Watanzania kwenye usimamizi wa rasilimali zao kwa kuwa ndizo pekee zinazochanganua mapato na matumizi ya bajeti na utekelezaji wake.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |