• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soko la madini laingiza mil. 300/- siku 20

    (GMT+08:00) 2019-05-24 20:15:33
    Soko la madini lililofunguliwa hivi karibuni wilayani Chunya, Mkoa wa Mbeya nchini Kenya limeanza kuleta manufaa baada ya serikali kukusanya kodi ya zaidi ya shilingi milioni 300 kutokana na mauzo ya dhahabu ndani ya siku 20 tangu soko hilo lifunguliwe.

    Soko hilo lilifunguliwa Mei 2, mwaka huu, kufuatia agizo ka Rais John Magufuli, alipokuwa kwenye ziara ya kikazi wilayani Chunya mwishoni mwa Aprili, ambapo alimwagiza Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Albert Chalamila, kuhakikisha soko hilo linafunguliwa huku akitahadharisha kuwa soko hilo ndilo jaribu la kibarua chake.

    Akizungumza juzi kwenye kikao na wakuu wa wilaya zote za Mkoa wa Mbeya na maofisa misitu, Chalamila alisema soko hilo limeleta manufaa makubwa kwa wachimbaji na serikali kutokana na kuingiza fedha nyingi.

    Alisema kilo 82 za dhahabu zimeuzwa katika soko hilo ndani ya siku 20, na kwamba uwapo wa soko hilo umeleta tija kubwa kwenye makusanyo ya kodi za serikali, tofauti na ilivyokuwa awali ambapo hapakuwapo takwimu za uhakika.

    Alisisitiza mapato ya aina hiyo yakikusanywa na kwenye vyanzo vingine ikiwamo mazao ya misitu na kilimo, serikali itakuwa na uwezo mkubwa wa kujitegemea katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

    Aliwataka wachimbaji wa dhahabu wilayani Chunya ambako ndio pekee madini hayo yanapatikana kwa Mkoa wa Mbeya, kuendelea kulitumia soko hilo pamoja na lililopo jijini Mbeya ili wanufaike zaidi na serikali ipate kodi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako