• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yachangia mchele kusaidia wahanga wa kimbunga Idai nchini Zimbabwe

  (GMT+08:00) 2019-05-25 17:15:16

  China jana ilichangia zaidi ya tani elfu kumi za mchele ili kusaidia watu walioathirika na kimbunga Idai pamoja na kaya zilizohatarini ambazo zinakabiliwa na njaa kutokana na ukame.

  Awali China ilichangia pesa taslimu dola laki 8 za Kimarekani kwa wahanga hao. Akikabidhi tani 10,165 za mchele kwa serikali ya Zimbabwe iliyowakilishwa na Waziri wa Huduma za Umma, Kazi na Ustawi wa Jamii Sekesai Nzenza, naibu waziri wa biashara wa China Qian Keming ambaye yupo ziarani nchini humo amesema China imedhamiria kuisaida Zimbabwe kupambana na balaa la njaa kupitia kuongeza uzalishaji wake kwenye kilimo na kutoa msaada wa dharura wa chakula unapohitajika.

  Kwa upande wake Bi Nzenza ameishukuru China kwa mchango wake na kusisitiza kuwa serikali yake bado inahitaji msaada zaidi ili kukabiliana na athari kubwa ya kimbunga.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako