• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mkutano wa UN wasambaza nyaraka za mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja"

  (GMT+08:00) 2019-05-25 18:12:14

  Mkutano wa Umoja wa Mataifa jana ulisambaza hotuba ya rais Xi Jinping wa China aliyoitoa kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja" na taarifa ya pamoja ya mkutano huo, na kufanya kuwa nyaraka rasmi za Umoja wa Mataifa.

  Mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja" ulifanyika kuanzia Aprili 24 hadi 27 hapa Beijing. Baada ya mkutano huo, balozi wa kudumu wa China kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Ma Zhaoxu alimwandikia barua katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Antonio Guterres akimuomba isambazwe hotuba ya rais Xi Jinping wa China aliyoitoa kwenye ufunguzi wa mkutano wa pili wa baraza la kimataifa la ushirikiano wa "Ukanda mmoja, Njia moja" na taarifa ya pamoja ya mkutano huo, na kufanywa kuwa nyaraka rasmi za Umoja wa Mataifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako