• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais Xi Jinping atuma barua ya pongezi kwenye maonesho ya kimataifa ya Big Data ya China

  (GMT+08:00) 2019-05-26 17:57:43

  Rais Xi Jinping wa China ametuma barua ya pongezi kwenye maonesho ya kimataifa ya mwaka 2019 ya Big Data yaliyofunguliwa mjini Guiyang, Mkoani Guizhou.

  Kwenye barua yake Rais Xi amesema teknolojia ya kizazi kipya ya mawasiliano ya habari, yenye internet, Big Data na akili bandia, inaendelea kukua na imekuwa na mchango mkubwa kwenye maendeleo ya uchumi, maendeleo ya kijamii na maisha ya watu katika nchi zote.

  Rais Xi amesema nchi mbalimbali zinatakiwa kuimarisha ushirikiano, kuongeza mabadilishano na kutumia fursa kidigitali za internet, na kushughulikia vizuri changamoto za kisheria, usalama na usimamizi wa sekta ya big data.

  Rais Xi pia amesema anatumai washiriki watajadili mipango ya maendeleo ya sekta hiyo na ushirikiano, ili kuchangia maendeleo ya nchi zote na kujenga jumuiya ya binadamu yenye mustakbali wa pamoja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako