• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanadiplomasia wa nchi za Afrika watumai kuwepo ushirikiano zaidi na China soko huria la Afrika linapoanza kufanya kazi

  (GMT+08:00) 2019-05-26 17:58:32

  Wanadiplomasia na maofisa wa nchi za Afrika wamepongeza uhusiano uliopo kati ya China na nchi zao, na kutumai kuwa kutakuwa na ushirikiano zaidi kati ya pande hizo wakati soko huria la bara la Afrika linapokaribia kuanza kazi.

  Akiongea jana wakati wa maadhimisho ya siku ya Afrika, kiongozi wa mabalozi wa nchi za Afrika ambaye pia ni balozi wa Cameroon nchini China Bw. Martin Mpana, amepongeza uhusiano kati ya China na Afrika na kusema unagusa karibu maeneo yote ya maendeleo.

  Amesema alama za miradi ya China zinaonekana kila mahali barani Afrika ikiwa ni pamoja na kwenye miradi ya ujenzi wa barabara, majengo, uchimbaji wa madini, maji na usafi.

  Mjumbe wa Umoja wa Afrika nchini China Bw. Rahamtalla Osman, amesema Afrika inaitegemea China, na uhusiano kati ya pande mbili ni wa kunufaishana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako