• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kampuni ya Huawei ya China kuhimiza maendeleo ya miji ya kisasa barani Afrika

  (GMT+08:00) 2019-05-27 08:31:03

  Kampuni ya mawasiliano ya simu ya China Huawei inatarajia kuhimiza maendeleo ya miji ya kisasa barani Afrika ili kuchangia mazingira endelevu.

  Mkurugenzi mwandamizi wa mambo ya umma wa Kampuni hiyo nchini Kenya Bw. Adam Lane ameliambia shirika la habari la China Xinhua kuwa miji ya Afrika inaweza kutumia teknolojia za kisasa kwenye nyanja za matumizi ya maji na nishati, mawasiliano, na maboresho ya usalama.

  Akiongea kwenye Mazungumzo ya Viongozi wa Biashara kabla ya Kikao cha Kwanza cha Baraza la UN-Habitat, Bw. Lane amesema Huawei inafanya mazungumzo na baadhi ya miji ya Afrika ili kueneza dhana ya Miji ya Kisasa, na kampuni hiyo imeshatumia teknolojia za kisasa katika miji ya Kenya, Nigeria na Botswana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako