• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania yauza dhahabu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 14 ndani ya mwezi mmoja

  (GMT+08:00) 2019-05-27 08:47:26

  Waziri wa madini nchini Tanzania Bw. Dotto Biseko amesema, Tanzania imeuza dhahabu yenye thamani ya dola za kimarekani milioni 14 ndani ya mwezi mmoja kwenye vituo 21 vya biashara ya dhahabu vilivyozinduliwa karibuni nchini humo.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Idara ya Habari (Maelezo) nchini humo, Bw. Biseko ameeleza matarajio yake kuwa uuzaji wa dhahabu kwenye vituo hivyo utasaidia kuhimiza ongezeko la uchumi wa nchi hiyo.

  Mwezi Aprili, rais John Magufuli aliwaelekeza makamishna wa mikoa inayozalisha madini kufungua vituo vya biashara ya madini. Amesisitiza kuwa vituo hivyo vinasaidia kuzuia magendo ya dhahabu kwenda nje ya nchi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako