• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la mpito la kijeshi la Sudan lasema majadiliano na upinzani yanaendelea taratibu

  (GMT+08:00) 2019-05-27 08:48:59

  Baraza la Mpito la Kijeshi la Sudan limesema majadiliano na makundi makuu ya upinzani kuhusu kuhamisha madaraka yanaendelea taratibu.

  Msemaji wa Baraza hilo Shams-Eddin Kabashi amesema, kasi ya majadiliano hayo ni ndogo, na kama hali itaendelea hivyo, inaweza kuleta maamuzi kadhaa yanayosimamia matakwa ya wananchi wa Sudan na usalama wa nchi hiyo. Amesisitiza tena nia thabiti ya Baraza hilo ya kukabidhi madaraka kwa raia, akisema baraza la kijeshi linawakilisha jeshi la ulinzi na majeshi mengine ya kawaida, na ni mhakikishaji mkuu wa utulivu wa nchi.

  Wakati huohuo, mwenyekiti wa Baraza hilo Abdel Fattah al-Burhan amekwenda Falme za Kiarabu (UAE) kwa ziara rasmi ya siku moja.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako