• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Somalia yaupongeza Umoja wa Afrika kwa juhudi zake kwenye operesheni za kulinda amani

  (GMT+08:00) 2019-05-27 08:53:33

  Waziri wa ulinzi wa Somalia Bw. Hassan Ali Mohamed jana ameipongeza tume ya Umoja wa Afrika nchini Somalia AMISOM kwa juhudi zake kwenye kurejesha amani na usalama nchini humo.

  Bw. Ali Mohamed alisema hayo mjini Mogadishu alipohutubia hafla ya kusherehekea Siku ya Afrika. Amesema lengo moja la kuanzisha Umoja wa Afrika ni kutoa mchango katika operesheni za kulinda amani barani Afrika, na AMISON ni mfano mzuri wa manufaa ya Umoja wa Afrika. Ameipongeza tume hiyo kwa kazi zake katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyodumu kwa miongo kadhaa nchini Somalia, ambavyo vimeiharibu nchi hiyo na kuwafanya wananchi wake wakimbie makwao.

  Amesisitiza kuwa nchi za Afrika lazima zitatue suala la wakimbizi, ili kusaidia kuwazuia vijana wa Afrika kukimbilia Ulaya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako