• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yakanusha kufanya mazungumzo na Marekani kuhusu mvutano

    (GMT+08:00) 2019-05-27 09:56:27

    Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran imekanusha ripoti zilizotolewa na vyombo vya habari vya Kuwait kwamba nchi hiyo ilianza mazungumzo na Marekani juu ya mvutano kati yao. Msemaji wa Wizara hiyo Abbas Mousavi amesema hakuna mazungumzo yoyote, iwe ya moja kwa moja ama yasiyo ya moja kwa moja kati ya nchi hizo mbili. Wakati huohuo, Shirika la Habari la Iran IRNA limeripoti kuwa, rais Hassan Rouhani amesema Marekani inatoa shinikizo kubwa lisilo na mfano kwa Iran, na kwamba meli za kusafirishia mafuta za Iran zinafuatiliwa na satelaiti za Marekani na zinashindwa kutia nanga katika bandari ya nchi yoyote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako