• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UGANDA: Vijana wakupambatia kilimo Tanzania

    (GMT+08:00) 2019-05-27 18:52:54

    Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, ameelezea kufurahishwa na kasi ya vijana nchini kujiunga na kujishughulisha na kilimo tofauti na siku za nyuma, ilivyo kuwa vigumu kuwashawishi vijana kuchangamkia kilimo. Waziri aliyasema haya wikendi alipokuwa akifungua Jukwaa la Fikira la Mwananchi, lililofanyika katika ukumbi wa Kisenga jijini Dar es Salaam. Takwimu za mwaka wa 2014 za Integrated Labour Force Survey, zinaonyesha kwamba vijana ni asilimia 56 ya nguvu ya taifa, hivyo wakihusishwa na kuwezeshwa ipasavyo kwa kuwavutia kwa kuzingatia mahitaji yao ya msingi katika kuwekeza kwenye kilimo, watalifikisha taifa katika maendeleo chanya. Waziri aliongeza kuwa Wizara ya Kilimo ina Mkakati wa Taifa wa Vijana wa kuwawezesha kushiriki katika kilimo kwa kuzingatia malengo makuu 10 yakiwemo upatikanaji wa ardhi, upatikananji wa mitaji, mafunzo ya ujasiriamali na uhakika wa masoko ya bidhaa zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako