• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • KENYA:Mkurugenzi mkuu wa KQ kujiuzulu

    (GMT+08:00) 2019-05-27 19:07:31

    Huenda misukosuko inayoikumba Shirika la ndege la KQ zimechangia mkurugenzi mkuu wake kutangaza rasmi kuwa atajiuzulu ifikapo Desemba tarehe 31 mwaka huu. Mkurugenzi huyo mkuu Sebastian Mikosz anasema kwamba anakatiza kandarasi yake ya miaka mitatu kwa sababu zake binafsi. Mweneyeki wa KQ Michael Joseph alisema kwamba ni kweli amepokea ombi la mkurugenzi mkuu la kujiuzulu mwishoni mwa mwaka huu. Bwana Mikosz ambaye ni mzawa wa Poland, aliajiriwa mwezi Juni mwaka wa 2017 na awamau yake afisini ilikuwa ikamilike mwezi Juni mwaka ujao.. Akiwa afisini, shirika la kQ liliandikisha hasara ya shilingi bilioni 7.55 mwaka wa 2018.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako