• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaboresha ulinzi wa haki za watoto kwenye maeneo yenye watu maskini

    (GMT+08:00) 2019-05-27 19:55:14

    Serikali ya China imeimarisha ulinzi wa watoto walioachwa nyumbani na wazazi waliohamia kufanya kazi mijini, na wale wa maeneo yenye watu maskini, wakati China ikiendelea kupambana na umaskini.

    Naibu mkurugenzi wa idara ya ustawi wa watoto ya wizara ya mambo ya kiraia ya China Ni Chunxia, amesema kwa mara ya kwanza wizara hiyo imetenga dola milioni 58 kwa ajili ya ulinzi wa watoto kutoka kwenye mfuko wa taifa kwa ajili ya watoto wenye changamoto za kifedha.

    Mfuko huo utatumika kukusanya ushahidi kuhusu watoto wanaotakiwa kuokolewa, kuchunguza walezi wao, na kufanya ufuatiliaji na kuwatembelea mara kwa mara watoto wenye mahitaji.

    Idara hiyo imesema katika muda wa miaka miwili iliyopita, asilimia 70 ya msaada umetolewa kwa mashirika ya watoto kwenye maeneo maskini.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako