• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu 5,750 wahukumiwa kwa kufanya uonevu shuleni tangu mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2019-05-27 19:58:11

    Idara kuu ya kuendesha mashtaka ya China imesema watu 5,750 wamehukumiwa kutokana na vitendo vya uonevu shuleni tangu mwaka 2018, wakati huo huo mkuu wa idara ya kuendesha mashtaka dhidi ya wahalifu watoto Bw. Shi Weizhong amesema watu wengine 3,407 walikamatwa.

    Mbali na hilo idara hiyo pia imesaidia kuboresha usimamizi wa usalama kwa shule na kutoa mapendekezo 3,472 kuhusu usalama vyuoni tangu mwaka 2018.

    Idara za kuendesha mashtaka pia zimetoa mihadhara vyuoni zaidi ya elfu 51 kuhusu utawala wa kisheria tangu mwaka jana, kwa shule elfu 57, na kuhusisha walimu na wanafunzi milioni 38.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako