• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawasiliano kati ya watu hayapaswi kutiwa mambo ya kisiasa

    (GMT+08:00) 2019-05-27 20:02:45

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo amesema, mawasiliano ya watu yanaendana na maslahi ya pamoja ya watu wa China na Marekani, na hayapaswi kutiwa mambo ya kisiasa na kuzuiwa.

    Bw. Lu Kang amesema China imefuatilia taarifa husika iliyotolewa na mkuu wa Chuo Kikuu cha Yale cha Marekani Bw. Peter Salovey. Katika mwaka huu vyuo vikuu vingi vikiwemo vyuo vya Yale, Stanford, California na Berkeley, vimetoa taarifa kueleza uungaji mkono kwa wanafunzi na wasomi kutoka nchi za nje wanaosoma Marekani, wanaona mashaka yanayotokana na uraia huenda yanasababishwa na kutokuwa na usawa.

    Bw. Lu Kang amesema China siku zote inaona mawasiliano ya watu ni msingi wa kuhimiza maingiliano na ushirikiano wa sekta mbalimbali kati ya China na Marekani, yanaendana na maslahi ya pamoja ya watu wa nchi hizo mbili, hayapaswi kutiwa mambo ya kisiasa na kuzuiliwa. China inatumai serikali ya Marekani itaheshimu maoni ya raia, na kufanya mambo yanayosaidia kuongeza maelewano na urafiki kati ya watu wa nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako