• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya kuandikisha wasafirishaji wote wa mizigo inayotoka na kuingia nchini humo ili kuwanasa wakwepa kodi

    (GMT+08:00) 2019-05-28 08:34:33

    Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema serikali yake itawahakiki na kuwaandikisha wasafirishaji wote wa mizigo inayotoka na kuingia nchini humo ili kuwanasa wakwepa kodi.

    Baada ya ziara ya pili ya ghafla katika kituo cha kuhifadhi makontena ICD mjini Nairobi ndani ya siku mbili, rais Kenyatta amesema ni wasafirishaji walioandikishwa baada ya mchakato wa kuwahakiki ndio wataruhusishwa kufanya kazi na wafanyabiashara ndogondogo ya kuingiza na kuuza bidhaa nje, ili kuepusha kuchelewa kupitishwa kwa makontena katika kituo hicho.

    Rais Kenyatta amewahakikishia wafanyabiashara wadogo kuwa bidhaa zao zitapitishwa kwa wakati kama wakifuata taratibu, na pia amewaonya waingizaji bidhaa kuwa serikali itazidisha juhudi zake za kuzuia uingizaji wa bidhaa feki nchini humo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako