• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bodi ya Uchaguzi ya Ethiopia yahitaji dola milioni 129 za kimarekani kuendesha uchaguzi wa mwaka 2020

    (GMT+08:00) 2019-05-28 08:34:53

    Bodi ya Uchaguzi ya Taifa ya Ethiopia NEBE imetangaza kuwa inahitaji dola za kimarekani milioni 129 kwa ajili ya kuendesha uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka 2020.

    Akizungumza na wanahabari, mwenyekiti wa bodi hiyo Bibi Birtukan Mideksa amesema bodi yake inaliomba bunge la Ethiopia kutenga fedha zinazohitajika kwa ajili ya uchaguzi huo. Amesema bodi yake imeendelea na juhudi zake za kuufanya uchaguzi mkuu ujao uwe wa haki na huru, ikiwemo kurekebisha kanuni za bodi, kufanya mageuzi ya kitaasisi na kuandaa mikutano ya vyama vya kisiasa.

    Ethiopia inapanga kufanya uchaguzi wa bunge na serikali za mitaa mwezi Mei mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako