• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya afya ya Rwanda yataka polisi waunge mkono kupiga marufuku ya uvutaji wa sigara kwenye maeneo ya umma

    (GMT+08:00) 2019-05-28 08:51:42

    Wizara ya afya ya Rwanda jana imewataka polisi nchini humo na taasisi husika ya usimamizi kusaidia katika kutekeleza sheria ya kupiga marufuku uvutaji sigara kwenye maeneo ya umma.

    Sheria ya udhibiti wa tumbaku nchini Rwanda iliyotangazwa mwaka 2013 ilipiga marufuku uvutaji wa sigara kwenye maeneo ya umma, na iliwataka wamiliki wa mikahawa, hoteli na maeneo mengine ya umma kutenga maeneo maalumu ya kuvuta sigara.

    Taarifa iliyotolewa na wizara ya afya ya Rwanda imesema, sheria hiyo bado haiwazuii watu kuvuta sigara kwenye maeneo ya umma, na hoteli, mikahawa na baa nyingi hazijatekeleza agizo hilo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako