• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zimbabwe yasema wauzaji bidhaa nje wameweka dola milioni 900 za kimarekani kwenye akaunti za benki nje ya nchi

    (GMT+08:00) 2019-05-28 09:05:44

    Zimbabwe haijapokea dola milioni 900 za kimarekani inazodai kutokana na uuzaji wa bidhaa nje ya nchi katika miezi 17 iliyopita, wakati ambapo nchi hiyo inakabiliwa na uhaba mkubwa wa fedha za kigeni.

    Katibu mkuu wa Wizara ya Fedha Bw. George Guvamatanga ameiambia kamati ya bunge ya bajeti na fedha kuwa, biashara ya nje ya nchi hiyo kwa mwaka 2018 ilifikia dola bilioni 1.4 za kimarekani, na kati ya hizo, dola milioni 500 bado hazijalipwa.

    Amesema kati ya mwezi Januari hadi Mei mwaka huu, uuzaji nje wa bidhaa wa nchi hiyo ulifikia dola za kimarekani bilioni 1.4, na mpaka sasa dola milioni 400 bado hazijalipwa. Pia ameongeza kuwa, dola nyingine milioni 800 bado zipo kwenye akaunti za nchi za nje za wauzaji wa bidhaa nje ya nchi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako