• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Bustani ya Viwanda iliyojengwa na China nchini Ethiopia yavutia makampuni ya kimataifa ya madawa

    (GMT+08:00) 2019-05-28 09:06:02

    Serikali ya Ethiopia imesema, Bustani ya Viwanda ya Kilinto iliyojengwa na kampuni ya China imeboresha nia ya nchi hiyo ya kuvutia kampuni za kimataifa za madawa duniani.

    Tume ya Uwekezaji ya Ethiopia (EIC) imesaini makubaliano ya uwekezaji na kampuni 10 za kimataifa ambazo zimeonyesha haja kubwa ya kufungua viwanda vyao ndani ya Bustani hiyo. Pia Tume hiyo imesisitiza kuwa, bustani hiyo ya viwanda, mara itakapotumika kikamilifu, itaongeza uwezo wa nchi hiyo kuvutia kampuni zaidi za kigeni katika sekta ya madawa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako