Shirika la Afya Duniani WHO limesema watu 562 wameuawa na wengine 2,855 kujeruhiwa katika mapigano ndani na karibu na mji mkuu wa Libya, Tripoli. WHO imeongeza kuwa kati ya watu waliouawa, kuna wafanyakazi wawili wa afya. Jeshi lenye makao makuu mashariki mwa nchi hiyo linaloongozwa na Khalifa Haftar limekuwa likifanya kampeni ya kijeshi tangu mapema mwezi Aprili ili kudhibiti mji wa Tripoli, ambao ni makao makuu ya serikali inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |