• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Namibia yatoa wito kwa Tanzania kufanya juhudi za pamoja ili kupambana na umaskini

    (GMT+08:00) 2019-05-28 09:13:00

    Rais Hage Geingob wa Namibia ametoa wito kwa Tanzania kufanya juhudi za pamoja ili kuboresha maisha ya watu wa pande hizo mbili.

    Rais Geingob amesema hayo alipokutana na rais John Magufuli wa Tanzania ambaye yupo ziarani nchini humo. Amesema, Namibia na Tanzania zinakabiliwa na changamoto za pamoja za maendeleo kama vile umaskini na ukosefu wa ajira. Pia amesema jukumu la nchi hizo mbili ni kuimarisha jitihada kwa lengo la kukomesha umaskini, kuleta maendeleo endelevu na kudumisha amani na utulivu.

    Rais Geingob ameongeza kuwa, ana imani kuwa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili utaleta matokeo mazuri, ikiwa zitatafuta mageuzi, kukuza uchumi na kuimarisha ushirikiano kati ya pande mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako