Shirika la Umoja wa Mataifa la idadi ya watu (UNFPA) linashirikiana na Sudan Kusini kuimarisha mfumo wa sheria ili kusaidia kupambana na ukatili wa kijinsia.
Mwakilishi wa shirika hilo nchini Sudan Kusini Bi. Mary Otieno amesema, nchi hiyo inahitaji sheria ya kitaifa inayounganisha pamoja sheria zote tofauti na kanuni za adhabu zinazohusiana na unyanyasaji wa kijinsia.
Bi. Otieno amesema, UNFPA, wizara ya ustawi wa jamii, jinsia na watoto, kwa kushirikiana na wizara ya sheria na mambo ya kikatiba wameanza mchakato wa kuunda mfumo bora wa sheria wa kukabiliana na unyanyasaji wa kijinsia nchini humo.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |