• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mswada wa kodi ya kaboni waleta mvutano nchini Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2019-05-28 09:30:58

    Mswada wa sheria wa kodi ya kaboni ambao umesainiwa na rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini kuwa sheria rasmi, umepokelewa kwa maoni tofauti, wakati baadhi ya watu wakiwa na wasiwasi kwamba wateja wataweza kulipia gharama na wengine wakishangilia njia hiyo itasaidia kulinda mazingira.

    Mkuu wa chuo cha sayansi ya kiuchumi na kibiashara cha Chuo Kikuu cha Wits Bw. Jannie Rossouw amesema, wateja wa kiwango chochote watagundua kuwa watalipa zaidi wakati sheria hiyo itakapotekelezwa. Amesema, wakati kodi moja ikiongezeka, wateja watalipa zaidi, na hii itaonekana kwa kupanda kwa bei za bidhaa, hivyo mfumko wa bei utaongezeka kufuatia kutozwa kwa kodi.

    Wakati huohuo, mbunge anayewakilisha Muungano wa Vyama vya Wafanyakazi nchini Afrika Kusini (COSATU) Bw. Matthew Parks amepongeza sheria hiyo wakati athari za mabadiliko ya hali ya hewa zikionekana kidhahiri.

    Afrika Kusini ni moja ya nchi zinazotoa hewa nyingi zaidi ya kaboni barani Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako