• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Japan na Marekani zashindwa kufikia mwafaka katika mazungumzo ya biashara

    (GMT+08:00) 2019-05-28 09:52:44

    Waziri mkuu wa Japan Abe Shinzo na rais Donald Trump wa Marekani wamekutana mjini Tokyo, na kukubaliana kukuza uhusiano wa kiwenzi kati ya nchi zao. Lakini viongozi hao wameshindwa kufikia maoni ya pamoja juu ya masuala wanayofuatilia kwa pamoja yaliyopo kwenye mazungumzo ya biashara kati ya Japan na Marekani.

    Baada ya mazungumzo yao, Abe amesisitiza mchango mkubwa uliotolewa na kampuni za Japan kwa uchumi wa Marekani, na ameeleza matumaini yake kuwa, uchumi wa nchi hizo mbili utaendelezwa zaidi. Naye rais Trump amesema biashara isiyo na uwiano imekuwepo kati ya Marekani na Japan kwa miaka mingi, na anatarajia kuwa nchi hizo zitafikia makubaliano yanayonufaisha pande zote kwenye mazungumzo ya biashara.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako