• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya Mambo ya Nje ya China yajibu kauli ya Marekani kwamba haijako tayari kufikia makubaliano ya biashara na China

    (GMT+08:00) 2019-05-28 10:21:17

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesisitiza kuwa China siku zote inashikilia msimamo kwamba tofauti yoyote kati ya nchi mbili ikiwemo migogoro kati ya China na Marekani katika sekta ya uchumi na biashara, inatakiwa kutatuliwa kwa mazungumzo ya kirafiki.

    Lu Kang amesema hayo ikiwa ni majibu kwa kauli iliyotolewa jana na rais Donald Trump wa Marekani ambaye yuko ziarani nchini Japan, kuwa Marekani kwamba haijako tayari kufikia makubaliano ya biashara na China.

    Bw. Lu ameongeza kuwa, mazungumzo ya biashara kati ya China na Marekani lazima yazingatie kanuni za kunufaishana zikiwemo kuheshimiana na amani. Pia Lu alizungumzia makala iliyotolewa na Gazeti la New York Times inayosema vikwazo vilivyowekwa na Marekani dhidi ya Kampuni ya Huawei vimesababisha kukatishwa kwa ujenzi wa miundombinu kwenye maeneo ya vijijini nchini humo, akisema hatua zilizochukuliwa na Marekani zimeathiri maslahi ya viwanda na wateja nchini Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako