• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaipinga kithabiti Marekani kufanya mawasiliano yoyote ya kiserikali na Taiwan

    (GMT+08:00) 2019-05-28 10:21:23

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, China inapinga kithabiti Marekani kufanya mawasiliano yoyote ya kiserikali na Taiwan kwa kisingizio chochote, huku akiitaka Marekani ishughulikie masuala yanayohusiana na Taiwan kwa hatua mwafaka, ili kuepusha athari katika uhusiano kati ya China na Marekani na ushirikiano kati ya nchi hizo mbili katika sekta muhimu.

    Kauli hiyo imetokana na taarifa kuwa, Taiwan imedai kuwa msaidizi wa rais wa Marekani anayeshughulikia mambo ya usalama wa taifa Bw. John Bolton hivi karibuni alifanya mazungumzo na "ofisa mwenzake" wa Taiwan.

    Bw. Lu amesema, serikali ya Marekani inatambua wazi kuwa serikali ya Jamhuri ya Watu wa China ni serikali halali ya kipekee ya China na kuahidi kuwa mawasiliano kati yake na Taiwan hayatakuwa ya kiserikali, kwa hivyo ni kosa kumwita ofisa husika wa Taiwan ni "ofisa mwenzake" wa Bw. John Bolton.

    Amesisitiza kuwa sera ya uwepo wa China Moja ni msingi wa kisiasa kati ya China na Marekani, na China inapinga jaribio lolote la kutengeneza "China Mbili" au "Uwepo wa China Moja na Taiwan Moja".

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako