• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Atalanta yafuzu ligi ya mabingwa, AC Milan chali

    (GMT+08:00) 2019-05-28 10:32:11

    Atalanta imefuzu kwa mara ya kwanza kucheza ligi ya mabingwa tangu klabu hiyo ianzishwe baada ya kutoka nyuma na kuichapa Sassuolo kwa mabao 3-1.

    Baada ya kumaliza msimu huu kwa kishindo, ikiwemo kupata sare ugenini dhidi ya mabingwa Juventus, Atalanta imeandika rekodi kubwa msimu huu katika ligi ya Serie A.

    Mabao ya Duvan Zapata, Alejandro Dario Gomez na Mario Pasalic yalitosha kuihakikishia Atalanta kupata tiketi ya kucheza ligi ya mabingwa Ulaya kutokana na uzembe wa AC Milan.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako