• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • RIADHA: Murigi moto wa kuotea mbali mbio za milimani, ashinda Ufaransa

    (GMT+08:00) 2019-05-28 10:32:40

    Mkenya Lucy Wambui Murigi alifungua msimu wake wa kombe la dunia la mbio za milimani za mwaka huu kwa kushinda taji la Salomon Gore-tex Maxi-Race mjini Annecy nchini Ufaransa.

    Mbio hizi za umbali wa kilomita 16 na nusu zinahusisha wakimbiaji kupanda mlima mita 945 na kuteremka mita 990, zilishuhudia Murigi akitoa onyo mapema kwa wapinzani wake.

    Murigi alitumia saa 1:30:27 akijizolea alama 100 anazopata mshindi katika ligi hiyo ya mbio saba. McCormack alimaliza katika nafasi ya pili kwa saa 1:32:33 na kuvuna alama 90 naye Pessey akaridhika katika nafasi ya tatu kwa alama 85 baada ya kukamilisha mbio kwa saa 1:37:07.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako