• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Mataifa wapongeza mtindo wa maendeleo vijijini wa China unaopunguza umaskini

  (GMT+08:00) 2019-05-28 19:06:53

  Umoja wa Mataifa umepongeza mtindo wa maendeleo vijijini wa China unaopunguza umaskini na kubadilisha mwenendo wa watu kuhama kutoka vijijini kuhamia mijini.

  Mkuu wa kikanda na mipango miji wa Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa UN-Habitat Bw. Remy Sietchiping amesema mjini Nairobi kuwa, maendeleo ya kaunti ya Songyang katika mkoa wa Zhejiang, yameweza kubadilisha eneo la kijijini kwa kufuata njia za uvumbuzi za bei rahisi. Amesema maendeleo ya Songyang, ambalo ni eneo lililoko milimani, yanaonesha kuwa vijiji vinaweza kuwa na kiwango cha juu cha maisha.

  Meya wa Kaunti ya Songyang Bw. Wang Jun amesema ufufuaji wa maeneo ya vijijini kwenye kaunti hiyo, kuna lengo la kuweka uwiano kati ya mahusiano ya miji na vijiji, kupitia ujenzi wa makazi bora.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako