• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasema haitavumilia hata kidogo udanganyifu kuhusu data

    (GMT+08:00) 2019-05-28 19:07:16

    Idara ya takwimu ya taifa ya China imesema imezitaja na kuziaibisha mamlaka za baadhi ya sehemu kutokana na kuhusika na kuchakachua data, na kusema itaendelea kuwa na msimamo mkali kuhusiana na vitendo vinavyokwenda kinyume na sheria.

    Idara ya takwimu ya taifa NBS jana ilitaja matukio mawili kuhusiana na mkoa wa Yunnan, ambao maofisa wa huko waligundulika kupotosha takwimu kuhusu ufanisi wa viwanda. Kwenye wilaya za Luxi na Jianshui, wakaguzi waligundua kuwa maofisa waliingilia utoaji wa ripoti kuhusu takwimu.

    Hatua hiyo ni sehemu juhudi za serikali ya China kupambana na vitendo vya kuchakachua takwimu, wakati serikali inaweka mkazo kwenye uhalisi wa data.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako