• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Unilever yazindua mtambo wa kwanza wa umeme wa jua katika kiwanda cha chai cha Kericho

    (GMT+08:00) 2019-05-28 19:41:35

    Kiwanda cha chai cha Unilever mjini Kericho nchini Kenya kitaokoa gharama za umeem baada ya mtambo wa umeme wa jua wa kilowati 619 kusimikwa katika kiwanda hicho.

    Hii ni kupitia ushirikiano kati ya kampuni ya Unilever na ile ya CrossBoundary Energy.

    Kwa kuongeza umeme wa jua katika nguvu za umeme wa maji na majani ambazo kampuni hiyo inatumia,zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji ya nishati katika kampuni ya Unilever Tea yatakuwa yanashughulikiwa na nishati safi.

    Mkurugenzi Mkuu wa Unilever Tea Sylvia ten Den alisema mpango wao endelevu utapunguza gharama,utapunguza hatari na kujenga uaminifu na wadau wao.Alisema usimikaji wa umeme wa jua katika kiwanda chao cha Kericho unaonesha nia na kujitolea kwao katika kulinda mazingira na kutenegeza maisha mazuri kwa ajili ya vizazi vijavyo.

    Kampuni ya CrossBoundary Energy itaiuzia kampuni ya Unilever Tea umeme wa jua chini ya mkataba wa miaka 15.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako