• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • FedEx yasema vifurushi vya kampuni ya Huawei vyasafirishwa kwa makosa

    (GMT+08:00) 2019-05-28 20:43:24

    Kampuni ya FedEx ya Marekani nchini China, leo imetoa taarifa ikisema baadhi ya vifurushi vya kampuni ya Huawei vimesafirishwa kwa makosa. Kauli hiyo ni tofauti na taarifa zilizotolewa kwenye mtandao wa kijamii wa Weibo siku chache zilizopita.

    Habari mpya zinaonyesha kuwa, kampuni ya Huawei imetoa malalamiko kwa idara ya usimamizi wa posta ya China kuhusu tukio hilo.

    Habari kutoka shirika la habari la Reuters tarehe 24 zilisema, vifurushi viwili vya Huawei ambavyo vinasambazwa na Fedex kutoka Japan kwenda China vimesafirishwa kwenda Marekani, na Fedex pia inajaribu kusafirisha vifurishi vingine viwili vya Huawei kutoka Vietnam kwenda Marekani, ambavyo vingekwenda kwenye ofisi za sehemu nyingine za Asia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako