• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mhubiri wa Marekani ashindwa kwenye vita ya kisheria kuhusu kufungwa kwa redio nchini Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-05-29 08:50:10

    Mahakama Kuu mjini Kigali nchini Rwanda imekataa rufaa ya mhubiri wa Marekani Gregg Schoof, ambaye alizishtaki Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Umma nchini Rwanda (RURA) na Kamati ya Vyombo vya Habari ya Rwanda kwa kufuta leseni ya kituo chake cha redio .

    Kwenye mahubiri yaliyotangazwa na redio hiyo mwezi Januari mwaka 2018, mchungaji Nicolas Niyibikora alisema wanawake ni "chanzo cha uovu", maneno yaliyosambaa kwa kasi kwenye mitandao ya kijamii, na kusababisha hasira miongoni mwa wanaharakati wa haki za wanawake.

    RURA ilifuta leseni ya redio ya Schoof mwezi Aprili mwaka 2018, baada ya redio hiyo kushindwa kufuata masharti yaliyotakiwa ikiwemo kuomba msamaha kwa umma kwa kurekebisha vipindi vilivyorushwa na kulipa faini ya dola za marekani 2,331.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako