• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Tanzania afanya ziara ya siku mbili nchini Zimbabwe

    (GMT+08:00) 2019-05-29 08:50:32

    Rais John Magufuli wa Tanzania jana amewasili Zimbabwe na kuanza ziara rasmi ya siku mbili nchini humo.

    Rais Magufuli amewasili Zimbabwe akitokea Namibia, ambapo alifanya ziara ya siku mbili nchini humo, baada ya kuhudhuria sherehe ya kuapishwa kwa rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini Jumamosi iliyopita.

    Rais Emmerson Mnangagwa ambaye alimpokea mgeni wake kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Robert Gabriel Mugabe, alifanya ziara nchini Tanzania mwezi Juni mwaka jana, ambapo marais hao wawili walikubaliana kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya nchi hizo mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako