• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marais wa China na Niger wakutana Beijing

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:03:46

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na mwenzake wa Niger Mahamadou Issoufou mjini Beijing.

    Akizitaja China na Niger kuwa ni marafiki, wenzi na ndugu, rais Xi amepongeza kuimarishwa kwa hali ya kuaminiana kisiasa na mafanikio yaliyopatikana katika ushirikiano halisi kati ya nchi hizo mbili. Rais Xi amesema China iko tayari kushirikiana na Niger katika kutekeleza matokeo yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Kilele wa Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika uliofanyika Beijing, ili kuhimiza ushirikiano wa kimkakati kati ya pande hizo mbili na kuwanufaisha watu wa nchi mbili.

    Rais Xi amesisitiza kuwa China itaendelea kuiunga mkono Niger katika mapambano dhidi ya ugaidi kwa ajili ya amani na utulivu wa kikanda, na kuhimiza uungaji mkono wa Umoja wa Mataifa kwa kikosi cha pamoja cha Kundi la Nchi Tano za Sahel.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako