• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • AU na mashirika ya kikanda yataka suluhisho la ndani la masuala ya amani na usalama

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:23:05

    Wataalam wa amani na usalama wamekutana chini ya mwamvuli wa Umoja wa Afrika wakieleza wasiwasi wao juu ya kuongezeka kwa nchi za nje kuingilia nyanja ya amani na usalama wa Afrika.

    Taarifa iliyotolewa na Umoja huo jana imesema, wataalam hao wamesema hayo wakati wa mkutano wa kwanza wa mashauriano kati ya Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika na Mfumo wa Kikanda wa Kuzuia, Kudhibiti na Kutatua Migogoro.

    Washiriki wa mkutano huo wamesema hatua hiyo inahatarisha uwezo na juhudi na mapendekezo ya Afrika, na pia zinaweza kusababisha kuchelewa kwa utatuzi wa migogoro na mapigano katika bara hilo, hivyo kuleta athari mbaya kwa watu wa Afrika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako