• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sudan Kusini yazindua kituo cha kisasa cha kuhifadhi data

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:23:23

    Sudan Kusini imezindua kituo cha kisasa cha kuhifadhi data katika mji mkuu wa nchi hiyo, Juba, wakati nchi hiyo changa ikijitahidi katika ulinzi na usimamizi wa data na kuunga mkono miamala ya kifedha kupitia simu za mkononi.

    Mkurugenzi mtendaji wa Mamlaka ya Mawasiliano ya Taifa (NCA) nchini humo Lado Wani Kenyi amesema, kituo hicho kitasaidia nchi hiyo kurejea kutoka miaka mitano ya mapigano na kutimiza kujitegemea katika ulinzi na usimamizi wa data.

    Msaidizi wa waziri wa Habari na Utangazaji Justine Alier amesema, kituo hicho kitaboresha mazingira ya biashara na kuchochea kufufuka kwa uchumi wa nchi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako