• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • IGAD yahimiza ushiriki wa wanawake katika kuzuia mapambano

    (GMT+08:00) 2019-05-29 09:56:58

    Shirika la Maendeleo la Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki IGAD limehimiza nchi za Afrika Mashariki kuongeza nafasi ya wanawake katika kuzuia, kudhibiti na kutafuta suluhisho katika migogoro.

    Kauli hiyo imetolewa jana na mkuu wa kitengo cha upatanishi cha IGAD Bw. Aleu Garang, ambaye amesisitiza haja ya kuimarisha nafasi na ushiriki wa wanawake katika kanda hiyo, hususan nchini Sudan Kusini, Somalia na Sudan.

    Ameongeza kuwa ni kazi muhimu ya kuimarisha uwezo wa kuzuia, kudhibiti na kutafuta suluhisho la migogoro, inaweza kutekelezwa kiufanisi chini ya mfumo wa Azimio namba 1325 la Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa, ambalo linahimiza wanawake kushiriki kwenye mchakato wa amani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako